

Serikali imeweka wazi msimamo wake kuhusu hali ya kisiasa nchini, ikisisitiza kuwa hakuna sheria yoyote iliyovunjwa katika utekelezaji wa majukumu yake kama taifa huru linalozingatia utawala wa sheria.
Akizungumza na wahariri jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa serikali imekuwa wazi kuhusu masuala yote yanayohusu mwenendo wa kisiasa nchini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!