
Bunge la Ulaya limetoa maazimio kadhaa kwa Tanzania kuhusu sakata la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ambapo limeitaka serikali kumuachia huru mara moja bila masharti na kuhakikisha usalama wake.
Pia limezitaka mamlaka za Tanzania kusitisha kukamatwa kiholela kwa wapinzani, vitendo vya vurugu, mashambulizi na unyanyasaji dhidi ya wanachama wa upinzani, watetezi wa haki za binadamu, wanahabari na mashirika ya kiraia.
Pia limezitaka mamlaka hizo kuchunguza kwa uhuru ukiukwaji unaodaiwa kufanywa na polisi pamoja na matukio ya kutoweka kwa watu.

Pia limeitaka serikali kurekebisha sheria zake za makosa ya mtandaoni na za vyombo vya habari kuendana na sheria za kimataifa za haki za binadamu.
Pia limezitaka mamlaka za Tanzania kuirudisha Chadema kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Oktoba 2025 na kushirikiana na vyama vyote vya siasa.
Pia limeutaka Umoja wa Ulaya (EU) na nchi wanachama wake kushirikiana kwa makini na mamlaka za Tanzania kuhusu kesi ya Lissu na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!