Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

INEC Yakanusha Madaiwa ya Mfumo wa Uchaguzi Kuunganishwa na NIDA

  • 23
Scroll Down To Discover

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekanusha madai kwamba mfumo wake wa uchaguzi umeunganishwa na NIDA au chama cha siasa chochote. INEC imesisitiza kuwa uchaguzi unafanyika kwa njia za kawaida (manual) bila mtandao wowote wa kielektroniki na taasisi nyingine.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema wapiga kura hutumia kadi maalum ya kupigia kura pekee na majina yao husomwa hadharani kabla ya kuruhusiwa kupiga kura. Pia, vyama vya siasa na mawakala wao walikabidhiwa daftari la wapiga kura baada ya uboreshaji.

Tume imewataka wananchi kupuuza taarifa hizo za upotoshaji na kufuatilia taarifa sahihi kupitia vyanzo rasmi vya INEC, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.



Prev Post Rais Samia Aongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM
Next Post TRAMPA Yaonesha Matendo ya Huruma kwa Wagonjwa wa Kansa Ocean Road
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook