Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Jumatatu 05 May 2025

  • 35
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Jumatatu 05 May 2025

Katika tukio la kipekee linaloangazia nguvu ya uongozi wa wanawake na wahamiaji katika siasa za kimataifa, Faith Hewitt Kapilima, Mtanzania mwenye asili ya kabila la Wangoni kutoka Songea, amechaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya NNC nchini Uingereza kupitia chama cha kihafidhina cha Conservatives.

Safari yake ya kisiasa haikuwa rahisi, Faith alishiriki uchaguzi uliopita bila mafanikio, licha ya kuungwa mkono na viongozi wa juu wa chama chake, akiwemo Waziri na Mbunge wa eneo hilo. Hata hivyo, alikataa kukata tamaa.

Kwa kutumia uzoefu wake binafsi, mafunzo kutoka jamii ya Wangoni, na maadili ya kujitolea, Faith aliendeleza harakati zake kwa kampeni iliyojikita katika ujumbe wa: “Listening, Campaigning, Delivering.”

Akitangaza ushindi wake mnamo Mei 3, 2025, Faith alisema: “Kushindwa hakumaanishi mwisho. Ni hatua ya kujifunza na kukua. Kama binti kutoka Songea, najivunia kusimama mbele ya jamii kama mwakilishi, nikiwa na dhamira ya kusikiliza, kutetea na kutekeleza.”

Faith ameweka msukumo maalum katika ajenda za kijamii, ikiwa ni pamoja na huduma kwa watoto wenye ulemavu na upatikanaji wa huduma bora kwa jamii zilizopuuzwa kwa muda mrefu.

Ushindi wake unaakisi mabadiliko chanya katika siasa za mitaa na msukumo wa chama cha Conservative kukuza uongozi jumuishi.

Faith Kapilima sasa anachukuliwa kama mfano hai wa uongozi wa mabadiliko akitangaza kwa vitendo kwamba ndoto zinaweza kutimia, hata ukiwa mbali na nyumbani.



Prev Post Wachungaji Tanzania na Kenya, Watuma Neno Zito kwa Viongozi wa Dini
Next Post Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Serikali Haitavumilia Vitendo vya Kihalifu Dhidi ya Viongozi wa Dini
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook