Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wachungaji Tanzania na Kenya, Watuma Neno Zito kwa Viongozi wa Dini

  • 33
Scroll Down To Discover

Baadhi ya Wachungaji kutoka Tanzania na Kenya wa Kanisa la Wadventista Wasabato wakiwa katika maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania kwa ajili ya kuliweka katika mikono ya Mungu ili livuke salama katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.Maombi hayo yamefanyika katika Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wakihitimisha Wiki ya Uamsho.
VIONGOZI wa dini katika madhebu mbalimbali nchini wameshauriwa wasiwe wanasiasa wala kuwa sehemu ya wachochezi kwa kuwa wao ni sehemu ya kimbilio pindi nchi inapokuwa katika changamoto.
Aidha, wamekumbushwa wajibu wa kuiombea Tanzania hususan katika mwaka huu wa uchaguzi mkuu.
Hayo yameelezwa na wachungaji kutoka Tanzania na Kenya wa Kanisa la Wadventista Wasabato walipokuwa wakihitimisha Wiki ya Uamsho iliyokuwa na maombi mbalimbali ikiwemo kuiombea amani, umoja na mshikamano wa taifa.
Wiki ya Uamsho imeandaliwa na Kwaya ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) kutokea Kanisa la Wadventista Wasabato Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo katika maombi hayo pia wamewaalika wachungaji wa Kanisa hilo kutoka nchini Kenya.
Katibu wa Jimbo la Mashariki Kati mwa Tanzania wa Kanisa la Waadvestita Wasabato Tanzania Mchungaji Shashi Musa Wanna, amesema wamekuwa katika maombi kwa wiki nzima, pia wametumia nafasi hiyo kuwa na mahubiri pamoja.
“Tulikuwa na wiki ya uamsho wa kiroho katika kanisa letu lakini pia kuliombea taifa letu na wachungaji wenzetu kutoka Kenya ambao tulikuwa nao. Wenzetu wana uzoefu mkubwa wa mambo ya siasa yanayoendelea Kenya. Tumehimiza maombi na umuhimu wa amani katika nchi yetu.
Kwa upande wake Mhubiri kutoka Kenya, Mchungaji Patrick Muthee amesema katika zama hizi ambazo dunia imeharibika wakati mwingine makanisa na waumini wake wanajaribiwa huku akitahadharisha kuwa Kanisa linapoingia katika siasa ni changamoto kwa sababu roho ya Mungu inaondoka.
“Kazi ya Kanisa ni kuleta watu pamoja na tunatambua Mungu ndio huchagua viongozi sisi kama waumini Mungu anatutumia katika hali ile ya kupiga kura, lakini Mungu anajua njia iliyo bora. Hivyo Kanisa, viongozi, wachungaji na masheikh tuzungumze na waumini wetu,” amesema.
Kwa upande wake Mchungaji Haruni Muturi wa Kanisa la Wadventista Wasabato kutoka Kenya, amesema katika wiki ya uamsho wametumia nafasi hiyo kujihoji myoyoni na kujitoa upya kwa Yesu Kristo kwa sababu wanajua kuna majaribu.
“Kwa sababu ya majaribu hayo Mungu asikie watu wake na kuwarejesha katika upendo wake na jinsi tulivyokuwa tumekuja kuombea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hilo nalo ni jambo tumelizingatia sana,” amebainisha.
Awali Mchungaji wa Kanisa la Waadvestita Wasabato Kinondoni Victor Geofrey, ameeleza kuwa, wiki ya uamsho ilikuwa na lengo la kukumbushana mambo muhimu katika maisha ya Kikristo na kusimama kama Kristo alivyofundisha hususan wakijua wako kqtika siku za mwisho naye (Yesu Kristo) anakaribia kuja.
“Katika wiki ya uamsho pia tumeomba kwa mambo mbalimbali ya maisha ya kiroho lakini pia kwa ajili ya mambo ya taifa letu la Tanzania kwani tuko katika wakati ulio makini ambao kila Mtanzania anatakiwa kuchukua jambo hilo kwa umakini wake,” amesema.



Prev Post Vuna Zaidi ya Mamilioni na Meridianbet Leo
Next Post MAGAZETI ya Leo Jumatatu 05 May 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook