Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Katibu Mkuu Kiongozi Azindua Mwezi wa Elimu Kwa Shughuli za Wakaguzi wa Ndani

  • 32
Scroll Down To Discover

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Dkt. Moses Kusiluka, akizungumza na maafisa wa Taasisi za Umma na Binafsi kwenye kikao cha mwezi

KATIBU Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka ametoa wito kwa taasisis za Umma na Binafsi  kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuwaamini wakaguzi wa ndani ili kusadia kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kwa lengo la kusaidia kupunguza makosa yanayosababisha hati chafu na badala yake kuleta maendeleo chanya  katika taasisi na Taifa kwa Ujumla.

RAIS wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dk. Zelia Njeza (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka baada ya kufungua Mkutano wa Mwezi wa Ukaguzi wa Ndani uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma jana. Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa ndani, Benjamin Magai.

Balazi Dkt.KUSILUKA ameyasema hayo Jijini Dodoma kwenye kikao cha mwezi cha maaafisa ukaguzi wa ndani ambapo amesema ni muhimu kufanya kazi kwa kuzingatia welezdi na kufanya kazi kwa uwazi ili kufanikisha malengo ya taasisi na Taifa.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA) DKT. ZELIA NJEZA ameziomba  taasisi za Umma na Binafsi Nchini  kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa ndani ili wasaidie kuwapa Elimu juu uendeshaji wa  taasisi hizo ili zifanye kazi kwenye mlengo sahihi.



Prev Post Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo ya Askari Wapya 
Next Post Kiwanda Cha Nguzo Za Zege Tabora Kuzalisha Ajira, Kukuza Uchumi Wa Nchi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook