Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kiwanda Cha Nguzo Za Zege Tabora Kuzalisha Ajira, Kukuza Uchumi Wa Nchi

  • 43
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM kutakidhi mahitaji ya Mkoa wa Tabora na maeneo mengine ya jirani na kukuza uchumi wa nchi.

Kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha nguzo 120 kwa siku inadhihirisha kasi ya matumizi na uhitaji wa nguzo hizo za kisasa. Pia, makadirio yanaonesha kuwa, mahitaji yanaongezeka na hivyo kuongeza fursa kwa TCPM kulichangamkia soko hilo.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Aprili 3, 2025 mkoani Tabora mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM.

“Niwapongeze uongozi wa Kampuni ya TCPM na wadau wengine kwa jitihada zenu za kusimamia ujenzi wa Kiwanda hiki. Nimejulishwa kuwa utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 73. Ni matumaini yangu kuwa, asilimia iliyobaki mtaikamilisha kwa ufanisi na kwa kuzingatia muda na mahitaji yaliyopo,” amesema Dkt. Biteko.

Ameitaka TCPM kukamilisha mradi huo kwa kipindi cha miezi miwili iliyobaki, sambamba na kulielekeza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwapa TCPM shilingi bilioni 4 ili kukamilisha mradi kwa haraka kwa kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza wananchi wapate umeme.

Amesisitiza kuwa mahitaji ya umeme yanaongezeka kila mwaka kwa asilimia 10 hadi 15 ukuaji ambao unadhihirisha umuhimu na uhitaji zaidi wa miundombinu ya kisasa ikiwemo nguzo za zege ambazo ni mbadala wa nguzo za miti.

Ameitaka TCPM kujenga nguzo bora ili kuwa mfano kwa kampuni binafsi za kutengeneza nguzo.

Dkt. Biteko amebainisha manufaa ya Kiwanda hicho cha nguzo za zege kuwa kitachangia ukuaji wa ajira za moja kwa moja na ajira ambazo hutokana na mnyororo wa thamani.

Ametolea mfano “ Mwaka wa fedha uliopita 2023/2024 usambazaji ulikuwa nguzo 19,368. Lakini kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 hadi kufikia mwezi Aprili usambazaji wa nguzo ulifikia 34,181. Sawa na ongezeko la asilimia 76 ambayo hii tunaweza kusema ni ukuaji wa ajira ambayo itatengenezwa na Sekta hii ya usambazaji wa nguzo za zege,”



Prev Post Katibu Mkuu Kiongozi Azindua Mwezi wa Elimu Kwa Shughuli za Wakaguzi wa Ndani
Next Post Lissu Kuanza Mgomo wa Kula Kupinga Utaratibu wa Kesi Mahakamani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook