Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jenerali Mkunda Ahitimisha Mafunzo ya Askari Wapya 

  • 40
Scroll Down To Discover

Pwani: Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amehitimisha mafunzo ya Askari wapya katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi iliyopo Kihangaiko, Msata Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, Aprili 29 mwaka huu.
Askari waliohitimu mafunzo wamekula kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Mkunda amewataka Askari wapya kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiapo cha utii, na kuwajibika  kulinda mipaka ya nchi, kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Askari wapya wametakiwa kutunza afya zao   kwa kuwa muda wote wanatakiwa kuwa na utimamu wa afya ili waweze kulitumikia Taifa kama walivyokusudiwa.
Aidha, Jenerali Mkunda amewaasa Askari kuzingatia mambo manne kwa Mwanajeshi ambayo ni Nidhamu nzuri, Utii, Uhodari na Uaminifu kwani Taifa linawaamini na kuwategemea katika ulinzi.



Prev Post Benki ya Azania Yakabidhi Madawati 200 Kwa Shule za Msingi na Sekondari Musoma
Next Post Katibu Mkuu Kiongozi Azindua Mwezi wa Elimu Kwa Shughuli za Wakaguzi wa Ndani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook