MAGAZETI ya Leo Jumamosi 03 April 2025
Baada ya kikao kilichofanyika Dodoma, mji mkuu wa Tanzania, hatimaye Tanzania na Malawi zimekubaliana kuendelea na biashara kuanzia tarehe 02 Mei, 2025.
Nchi hizo mbili jirani zimesaini Tamko la Pamoja (Joint Communiqué) kufuatia kikao cha mawaziri wa Mambo ya Nje; Kilimo; Viwanda na Biashara wa pande zote.
Hatua hiyo inamaliza mvutano uliotokana na Malawi kuzuia mazao ya kilimo kutoka Tanzania, kabla ya Tanzania nayo kuchukua hatua kama hiyo kulinda maslahi yake.
Kusainiwa kwa Tamko la Pamoja kunarejesha na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo kulingana na mikataba na miongozo ya kikanda na kimataifa iliyopo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!