Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mchengerwa amshukuru Rais kwa kupandisha mishahara, Makonda Chapa Kazi

  • 30
Scroll Down To Discover

Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kupandisha kima cha chini cha mshahara wa watumishi wa Serikali kwa 35% Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amemshukuru na kuwaelekeza watumishi chini ya Wizara yake kuwa wazalendo na wabunifu ili kuinua uchumi wa nchi.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya Mei 2, 2025 wakati alipokuwa akiongea na watumishi wa Mkoa wa Arusha ambapo amesema Wizara yake inasimamia takribani asilimia 76 ya watumishi wote hivyo njia pekee ya kuunga mkono maono ya Rais ni kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

” Ndugu zangu ili tuweze kutekeleza maelekezo ya Rais wetu ni muhimu kutembea katika ndoto zake za kutaka kuwaletea watanzania maendeleo”. Amesisitiza Mchengerwa

Amesema kufuatia Rais kutoa ongezeko hilo la mshahara wa 35% Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi pekee ambayo imewapatia wananchi wake ongezeko kubwa barani Afrika.

Aidha, amewataka wataalam wa Serikali kwenye Halimashauri zote nchini katika mabaraza ya madiwani kusukuma ajenda za maendeleo na kuonya kwa baadhi ya watumishi wasio waadilifu kubadilika mara moja kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wa Wakurugenzi wa Halimashauri, amewataka kuendelea kusimamia miradi iliyopo kwenye maeneo yao kwa kuzingatia miongozo na sheria huku wakisahihisha makosa yaliyoainishwa ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Amewataka waongeze mifumo ya kupata taarifa za ubadhilifu na kuchukua hatua ili kuwadhibiti watumishi hao.

Amewapongeza kwa kazi nzuri ya kuongeza makusanyo na kuendelea kuminya mianya ya upotevu huku akiwataka kubuni vyanzo vipya.

Amewapongeza Wakuu wa Mikoa wote nchini kwa kuimarisha amani na kukuza uchumi kwa kusimamia vema miradi mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasisitiza kuendelea kufanya hivyo na kusisitiza kuwa kamwe siasa isiwe kikwazo cha kufanya maendeleo.

Pia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda kwa ubunifu wake na kumtaka asiyumbishwe na siasa.



Prev Post MAGAZETI ya Leo Jumamosi 03 April 2025
Next Post BoT yasisitiza marufuku matumizi ya fedha za kigeni kwenye miamala ya ndani Tanzania
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook