Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 02 May 2025

  • 27
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Ijumaa 02 May 2025

Shauri lililofunguliwa na Klabu ya Yanga katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) Kuomba Mechi ya Marudiano ya Ligi Kuu baina yao na Simba isipangiwe tarehe na pia ipewe pointi za mezani limegonga mwamba.

Mechi hiyo ilikuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu lakini ikaahirishwa baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, siku moja kabla ya mchezo.

CAS imeamua kutupilia mbali shauri hilo kwa vile Yanga haikufuata utaratibu wa kushughulikia malalamiko yake kwa kupeleka shauri hilo CAS kabla ya kuanza na vyombo vya ndani.

Katika majibu ya rufaa yake, CAS imeona haiwezi kuendelea na shauri hilo kwa vile Yanga haikufuata utaratibu kwa kufungua shauri kabla ya suala hilo kutolewa uamuzi na vyombo vya soka hapa nchini.

“Kwa hiyo, Naibu Rais anaona kuwa njia sahihi ya kukata rufaa ya Mrufani iko mbele ya Kamati ya Rufani ya TFF, na kwamba Mrufani alishindwa kutumia masuluhisho yote ya ndani ya kisheria kama inavyotakiwa na Ibara ya 37 ya Kanuni.

“Kwa hiyo, Naibu Rais anaona kwamba CAS haina mamlaka ya kutoa uamuzi kuhusu rufaa hiyo au kuhusu Ombi la Kutoweka lililowasilishwa na Mlalamikaji.

“Kwa kuzingatia hayo hapo juu, rufaa iliyowasilishwa na Young Africans Sports Club itachukuliwa kuwa imeondolewa na utaratibu wa CAS 2025/A/11298 Young Africans Sports Club dhidi ya Shirikisho la Soka Tanzania & Bodi ya Ligi Kuu Tanzania & Simba Sports Club utakatishwa na kufutwa kwenye orodha ya CAS,” imefafanua CAS.

Muda mfupi baada ya CAS kuamua hilo, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kujiandaa kupanga tarehe ya mechi hiyo, ambapo Kupitia Kurasa zake imeandika kuwa;

“Манакама ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imetupa rufani ya klabu ya Yanga yenye kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 ambayo klabu hiyo iliifungua dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC (Young Africans SC vs Simba SC).



Prev Post CCM Yalaani Vikali Shambulio Dhidi ya Katibu Mkuu wa TEC, Padre Kitima
Next Post Kwa Nini Wanawake Hawaruhusiwi Kuwa Papa Katika Kanisa Katoliki?
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook