MAGAZETI ya Leo Jumanne 29 April 2025
Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa ahadi ya Sh30 milioni kwa nyota wa Simba kwenye kila bao litakalofungwa kwenye mechi ya Fainali.
Simba inatarajia kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane baada ya kutinga hatua hiyo kwa kuifunga Stellenbosch ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Dk Samia anawapongeza Simba kwa kutinga hatua ya fainali na anawatakia kila la kheri kwenye mechi mbili za fainali zilizo mbele yao kwa kutoa ahadi ya kununua kila bao watakalofunga kwa Sh30 milioni.
“Mheshimiwa Rais anaamini Simba watabeba taji la michuano hiyo, anatambua kutakuwa na mechi mbili ya nyumbani na ugenini hivyo kwenye mechi zote kila bao watakaloshinda ni milioni 30,”
“Mkifunga moja milioni 30, mawili 60, matatu 90 manne Sh120 milioni, mama amefanya hivi kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wawe na morali, waweke juhudi kiwanjani na kushinda mechi zote mbili,” amesema Msingwa.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!