Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jaji Warioba Aanguka Wakati Akihutubia Mkutano

  • 1
Scroll Down To Discover

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameanguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini Tanzania, ambapo alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu.

Tukio hilo limetokea wakati wa mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), na kusababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda.

Kufuatia tukio hilo, Mwenyekiti wa TCD, Dorothy Semu, ametangaza mapumziko mafupi ili kuruhusu hali kutulia na hatua zinazohitajika kuchukuliwa.

Hadi sasa, taarifa zaidi kuhusu hali ya kiafya ya Jaji Warioba baada ya kuanguka kwake hazijawekwa wazi.

Mkutano huo ulikuwa ukijadili hali ya kisiasa nchini pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa demokrasia na siasa nchini Tanzania.

The post Jaji Warioba Aanguka Wakati Akihutubia Mkutano appeared first on Global Publishers.



Prev Post Dkt. Mwinyi Atoa Pole kwa Rais Samia Kufuatia Kifo cha Mumewe, Kuzikwa Leo Kizimkazi, Zanzibar
Next Post GBT Yatoa Wito Kwa Wachezaji Kucheza Kistaarabu na Ndani ya Uwezo Wao
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook