Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jordyn Lucas Aeleza Hisia Zake Baada ya Kukutana na Drake, Azawadiwa Mkoba wa Mil 66

  • 46
Scroll Down To Discover

Mrembo wa Marekani, Jordyn Lucas akionyesha mkoba aliozawadiwa na rapa maarufu Drake.

Mrembo wa Marekani, Jordyn Lucas, ametimiza ndoto yake ya muda mrefu baada ya kupata nafasi ya kukutana na rapa maarufu Drake.

Baada ya kukutana na msanii huyo, Jordyn anadaiwa kuondoka na zawadi ya dola 25,000 sawa na Sh milioni 66, pamoja na mkoba wa kifahari aina ya Birkin ambao alipewa na Drake.

Jordyn alionekana kufurahishwa na tukio hilo na kueleza hisia zake kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiambatanisha na video yao baada ya kukutana. Katika ujumbe huo, alionyesha mahaba ya kipekee kwa msanii huyo.

Jordyn alisema: “Mume wangu, mpenzi wangu, nguzo yangu ya maisha. Nimesubiri maisha yangu yote kwa ajili ya wakati huu na sasa imethibitishwa… tunastahili kuwa pamoja. Asante kwa Birkin yangu na dola 25,000, dada yangu.”

Kauli hiyo imezua gumzo mitandaoni, huku Jordyn akionekana kuufurahia sana mkutano wake na Drake pamoja na zawadi hizo anazodai kupewa na rapa huyo.

The post Jordyn Lucas Aeleza Hisia Zake Baada ya Kukutana na Drake, Azawadiwa Mkoba wa Mil 66 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Yanga Yapoteza Yanga Day, Mashabiki Wabaki na Furaha Baada ya Kuona Kiwango cha Timu
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 10, 2026 
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook