
Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, ameambatana na Madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Buchosa, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo (DED), Benson Peter Mihayo, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Isaac Mashimba, katika ziara ya kujifunza kuhusu ujenzi na uendeshaji wa masoko ya kisasa.
Ziara hiyo imefanyika katika Soko la Majengo jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa ahadi ya Mbunge huyo ya kujenga soko la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 4 ndani ya Jimbo la Buchosa.

Katika ziara hiyo, Shigongo akiwa pamoja na Madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Buchosa, wamekagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Majengo na kujifunza namna linavyoendeshwa na kusimamiwa.
Lengo ni kuhakikisha uzoefu na maarifa yatakayopatikana yanatumika katika utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa soko la kisasa katika Jimbo la Buchosa.
Shigongo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo la Buchosa, ikiwemo ujenzi wa soko hilo.
View this post on Instagram
The post Shigongo Aanza Safari Ya Soko La Kisasa La Bilioni 4 Buchosa – Video appeared first on Global Publishers.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!