Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

JKT Yaita Vijana 60,000 Waliohitimu Kidato Cha Sita Kujiunga Mafunzo ya Lazima

  • 11
Scroll Down To Discover

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza kuwaita vijana 60,000 waliomaliza kidato cha sita mwaka 2026 kujiunga na mafunzo ya lazima kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni ongezeko kutoka vijana 40,000 waliokuwa wakichukuliwa awali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Mei 28, 2026 kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Utawala Tawi la JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Juni 1 hadi 7, 2026 kwa ajili ya kuanza mafunzo rasmi.

Mabena amesema mpango huo unawahusu wahitimu wote wa kidato cha sita kutoka shule za Tanzania Bara na Zanzibar, huku akieleza kuwa mwelekeo wa baadaye ni kuhakikisha kila kijana anayehitimu elimu hiyo anapitia mafunzo ya JKT moja kwa moja.

“Sanjari na wito huo, JKT limewapangia makambi watakaokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti kambini kuanzia Juni 1 hadi 7, 2026,” amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Baadhi ya makambi yaliyotajwa kupokea vijana hao ni pamoja na Rwamkoma (Mara), Msange (Tabora), Ruvu na Kibiti (Pwani), Mpwapwa na Makutupora (Dodoma), Mafinga (Iringa), Male (Ruvuma), pamoja na Mgambo na Maramba mkoani Tanga.

Makambi mengine ni Makuyuni na Oljoro (Arusha), Bulombora (Kagera), Kanembwa na Mtabila (Kigoma), Itaka (Songwe), Luwa na Milundikwa (Rukwa), Nachingwea (Lindi) pamoja na Chuo cha Uongozi cha JKT Kimbiji kilichopo Dar es Salaam.

The post JKT Yaita Vijana 60,000 Waliohitimu Kidato Cha Sita Kujiunga Mafunzo ya Lazima appeared first on Global Publishers.



Prev Post Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Awasili Chato Kuhudhuria Mazishi ya Mama wa Hayati Magufuli
Next Post Rais Samia Asema Wananchi Bado Hawana Imani Kubwa na Polisi (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook