Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tyla Aingia Kwenye Playlist ya Barack Obama ya Msimu wa Kiangazi 2026

  • 148
Scroll Down To Discover

Nyota wa muziki kutoka Afrika Kusini, Tyla.

Nyota wa muziki kutoka Afrika Kusini, Tyla, ameendelea kung’ara kimataifa baada ya wimbo wake kuchaguliwa na aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, kuwa sehemu ya orodha yake ya nyimbo alizozipenda kwa msimu wa kiangazi 2026.

Obama aliuchagua wimbo wa Tyla unaoitwa “She Did It Again” akishirikiana na Zara Larsson, katika playlist yake yenye karibu nyimbo 50, ambayo aliielezea kuwa ni mkusanyiko wa muziki aliokuwa akiufurahia kipindi cha kiangazi.

Tyla si msanii pekee mwenye asili ya Afrika aliyepata nafasi kwenye orodha hiyo, kwani pia amejumuishwa msanii wa Ethiopia-Marekani Kelela kupitia wimbo “Idea 1”, pamoja na nyota wa Uingereza mwenye asili ya Ghana, RAYE, kupitia wimbo “Where Is My Husband!”

Playlist hiyo imejumuisha mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki kutoka kwa wasanii wakubwa kama Drake, SZA, Doechii, Coldplay, pamoja na nyimbo za kihistoria kutoka kwa The Beatles na David Bowie.

Hii si mara ya kwanza kwa Tyla kupata nafasi kwenye orodha ya muziki ya Obama, kwani mwaka 2024 pia alijumuishwa kupitia wimbo wake mkubwa wa kimataifa “Jump”.

Uteuzi huo unaendelea kuwa hatua nyingine kubwa katika safari ya Tyla, ambaye amekuwa miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaowakilisha vyema muziki wa bara hilo katika jukwaa la kimataifa.

The post Tyla Aingia Kwenye Playlist ya Barack Obama ya Msimu wa Kiangazi 2026 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Hamas yakubali kuweka chini silaha Gaza. Je, hii italeta amani Gaza? Katika Dira ya Dunia TV.
Next Post Matangazo ya Dira ya Dunia Redio 31/07/2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook