Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Awasili Chato Kuhudhuria Mazishi ya Mama wa Hayati Magufuli

  • 9
Scroll Down To Discover

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Chato Mkoani Geita, ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mazishi ya Marehemu Bi. Suzana Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yatakayofanyika tarehe 29 Mei 2026 Wilayani Chato.

Makamu wa Rais amepokelewa katika Uwanja wa Ndege Geita, Wilayani Chato, Mapokezi yaliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela, Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na Viongozi mbalimbali Waandamizi.

Pia Makamu wa Rais, amefika nyumbani kwa marehemu, Kilimani Chato kusaini kitabu cha maombolezo pamoja na kuwafariji wafiwa kufuatia msiba huo.

The post Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Awasili Chato Kuhudhuria Mazishi ya Mama wa Hayati Magufuli appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mashabiki wa Tyla Wapaniki Baada ya Kutoweka Mitandaoni Kabla ya APop
Next Post JKT Yaita Vijana 60,000 Waliohitimu Kidato Cha Sita Kujiunga Mafunzo ya Lazima
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook