KIKOSI cha Simba SC kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya B19 maarufu kama Mabeberu wa Jiji katika mchezo wa hatua ya 32 bora uliochezwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, na kufanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Simba ililazimika kupambana kwa nguvu ili kuvunja ukuta wa wapinzani wao ambao walionyesha kiwango kizuri tangu mwanzo wa mechi hiyo.
Bao la kwanza kwa Simba lilipatikana kupitia kwa mshambuliaji Inno Loemba aliyefunga kwa ustadi baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo Clatous Chama, na kuipa timu yake uongozi muhimu katika mchezo huo.
Baadaye katika dakika ya 77, Chama aliongeza bao la pili kwa Simba na kuzima kabisa matumaini ya B19 ya kurejea mchezoni, bao lililothibitisha ubora wa kikosi cha wekundu hao katika mchezo huo.
Kabla ya mchezo huo, mdhamini wa B19 alikuwa ameahidi kuwapatia magari wachezaji wa timu hiyo endapo wangefanikiwa kuifunga Simba na kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano hayo.
Ahadi hiyo iliongeza hamasa kubwa kwa wachezaji wa Mabeberu wa Jiji ambao waliingia uwanjani kwa ari ya kutafuta ushindi, wakiamini wanaweza kufanya maajabu dhidi ya wapinzani wao hao wakubwa.
Hata hivyo, ndoto hiyo haikutimia baada ya kocha wa Simba, Steve Barker, kupanga kikosi imara kilichoweza kudhibiti mchezo huo na hatimaye kuibuka na ushindi uliowanyima wapinzani wao nafasi ya kujinyakulia zawadi ya magari waliyokuwa wameahidiwa.
The post LOEMBA AFUNGUA NJIA, CHAMA AMALIZIA KAZI SIMBA appeared first on Soka La Bongo.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!