Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

YANGA KWENYE MTIHANI MZITO BILA NYOTA MUHIMU

  • 33
Scroll Down To Discover

KIKOSI cha Yanga SC kinashuka dimbani kesho kuwakabili Singida Black Stars, huku kikubwa cha changamoto za majeruhi kikizidi kuongezeka.

Kocha Mkuu wa kikosi cha Yanga, Pedro Goncalves, ameweka wazi kuwa timu inakabiliwa na wachezaji kujeruhiwa, lakini hilo halitawazuia kupambana kwa nguvu uwanjani.

“Changamoto za majeruhi ni kubwa, lakini wachezaji waliopo wanapaswa kujituma zaidi, kushirikiana kwa nidhamu, na kuhakikisha wanaitetea nembo ya klabu kwa nguvu zote,” amesema.

Pedro amethibitisha kuwa beki tegemeo, Dickson Job, ameumia na anatarajiwa kutohusika katika mechi kwa takriban miezi miwili, ingawa muda huo unaweza kubadilika kulingana na maendeleo ya matibabu yake.

Aidha, kiungo mshambuliaji, Pacome Zouzoua, bado hajarejea katika kiwango chake cha utimamu wa mwili kwa asilimia mia moja.

Licha ya changamoto hizo, kocha Goncalves ameonyesha imani kubwa kwa kikosi chake.

Amesema mshikamano, ari ya ushindi, na nidhamu ya wachezaji ndio vitakuwa nguzo kuu za kuhakikisha timu inashinda katika mtihani huu muhimu.

Yanga inashuka dimbani kwenye mchezo huo ikiwa na presha ya kutaka matokeo mazuri, huku mashabiki wakiwa tayari kushuhudia jinsi kikosi kilichopungukiwa nyota muhimu kitakavyopambana kwa nguvu na mbinu za kisasa.

The post YANGA KWENYE MTIHANI MZITO BILA NYOTA MUHIMU appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post DICKSON JOB NJE MIEZI MIWILI YANGA
Next Post NSAJIGWA, AZAM WAJE TUMALIZANE
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook