Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NMB YAIGEUZA NANENANE KUWA DARASA LA FURSA, MAARIFA NA UWEZESHAJI

  • 42
Scroll Down To Discover

DODOMA: Benki ya NMB imeendelea kuifanya Nanenane 2026 kuwa zaidi ya maonesho ya kilimo kwa kuendesha kampeni ya utoaji wa elimu ya kifedha, ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa wananchi waliotembelea mabanda yake katika kanda mbalimbali nchini.

Katika Banda la Vijana lililopo viwanja vya DK John Mwakangale jijini Dodoma, vijana wa mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) walipata mafunzo kuhusu namna ya kugeuza mawazo yao kuwa biashara endelevu, kusimamia fedha na kutumia huduma za kifedha kukuza shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Kilimo kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NMB, Christopher Mwalungenge, aliwahimiza vijana kuona kilimo kama biashara yenye fursa kubwa za kujenga kipato, ajira na ustawi wa muda mrefu.

Mbali na vijana, maafisa wa NMB waliendelea kutoa elimu kwa vikundi vya wakulima, wafugaji na wajasiriamali waliotembelea mabanda ya benki hiyo. Washiriki walipata uelewa kuhusu huduma za kifedha, mikopo ya sekta ya kilimo, bima pamoja na suluhisho zinazowawezesha kuongeza tija na kupanua biashara zao.

Kupitia elimu, ushauri na huduma za kifedha zinazotolewa katika mabanda yake, NMB imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama mshirika wa maendeleo ya wakulima, wafugaji, wavuvi na vijana, huku ikichochea uchumi jumuishi unaojengwa kupitia maarifa na uwekezaji wenye tija.



Prev Post LATRICIA SAWE AONDOKA KUIWAKILISHA TANZANIA MISS WORLD 2026 VIETNAM
Next Post Rais Samia Azindua Tume Maalum Kuchunguza Ghasia za Uchaguzi 2025 – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook