Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

PEDRO KUJA KIVINGINE ZANZIBAR, KAMWE ATOA ONYO

  • 23
Scroll Down To Discover

OFISA Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe, amesema kuelekea mchezo muhimu wa Jumapili, kocha wa kikosi hicho, Pedro Goncalves, ataonyesha sura tofauti ambayo wengi hawajawahi kuiona msimu huu watakapokutana na JS Kabylie.

Yanga watakuwa nyumbani katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar. Pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku kila timu ikihitaji matokeo chanya kumaliza hatua hiyo kwa heshima na nguvu.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi hicho, Kamwe amesema mechi hiyo ni ya kipekee na yenye uzito mkubwa kwa klabu, jambo linalompa kocha wao sababu ya kuingia na mbinu tofauti, mashabiki watashuhudia mabadiliko ya kimkakati na ushindani wa hali ya juu kutoka kwa benchi la ufundi.

“Katika haya mashindano kuna watu walisema sana juu ya kocha wetu Pedro kwamba anazoea kucheza kwa tahadhari. Mechi ya Jumapili ndio watakapokuja kuona sura yake tofauti na mechi zilizopita,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa mchezo huo ni muhimu kwa sababu Yanga inalenga kufuzu kwa kishindo na kwenda robo fainali ikiwa na morali ya juu. Kwa mujibu wa Kamwe, kikosi hicho kimejipanga kuhakikisha kinamaliza hatua ya makundi kwa matokeo yatakayothibitisha ubora wao.

“Sisi tayari tumeshacheza mechi zetu dhidi ya JS Kabylie, pamoja na zile za Al Ahly SC na AS FAR Rabat. Katika kundi hili, Yanga na Al Ahly ndio tunaelekea robo fainali,” ameongeza.

Katika Kundi B, anayeongoza ni Al Ahly kwa pointi 9, akifuatiwa na AS FAR Rabat mwenye alama 8, Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 5 huku JS Kabylie wakishika mkia kwa pointi 3.

Kutokana na umuhimu wa pambano hilo, Kamwe amesema hakuna Mwanayanga atakayebaki Dar es Salaam kwani mashabiki wengi wamejipanga kusafiri hadi Zanzibar kuipa sapoti timu yao.

Hata mfadhili wa klabu hiyo, Said Ghalib (GSM), anatarajiwa kuwasili visiwani humo kushuhudia timu ikisaka ushindi muhimu.

The post PEDRO KUJA KIVINGINE ZANZIBAR, KAMWE ATOA ONYO appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BAJABER TAYARI KUTIA NGUVU DHIDI YA STADE MALIEN
Next Post YANGA JIHADHARINI NYOTA WA SIMBA SC WANARUDI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook