Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA KUMLINDA MPANZU, KINACHOMTESA AHMED AFICHUA

  • 20
Scroll Down To Discover

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amevunja ukimya kuhusu hali ya kiungo wao, Elie Mpanzu, akieleza kuwa mchezaji huyo anapitia changamoto binafsi zinazomfanya ashindwe kuonyesha kiwango chake cha kawaida uwanjani.

Ahmed amesema Mpanzu yuko katika kipindi kigumu kutokana na masuala binafsi yanayomhusu, hali ambayo imeathiri utendaji wake ndani ya uwanja,  kuwa si rahisi kwa mchezaji kuwa katika ubora uleule kila wakati, hasa anapokumbwa na misukosuko ya maisha.

Amedai kuwa kuna watu kutoka upande wa pili wanajaribu kuleta taharuki kwa kumgombanisha mchezaji huyo na mashabiki, wakisambaza taarifa kwamba ana mapenzi na Yanga , jambo alilolitaja kuwa halina ukweli na lina lengo la kuvuruga umoja ndani ya klabu.

“Kuna watu wanamkosea sana Mpanzu. Anapitia wakati mgumu na kuna mambo binafsi yanayomhusu. Tukumbuke wiki iliyopita alifiwa na mtoto wake, akasafiri kwenda kwao DR Congo kwa mazishi na baadaye kurejea kuendelea na majukumu yake ya kazi,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa mbali na msiba huo mzito, ni kawaida kwa mchezaji kupitia vipindi vya kupanda na kushuka kwa kiwango. Hata hivyo, uongozi wa Simba una imani kubwa na Mpanzu na uko tayari kumvumilia huku ukimpa muda wa kurejea katika ubora wake.

Pia amebainisha kuwa kocha wa timu hiyo, Steve Barker, anatambua hali anayoipitia mchezaji huyo na amekuwa naye karibu, akimjenga kisaikolojia taratibu hadi atakapokuwa tayari kurejea katika kiwango chake bora.

Ahmed amewataka  mashabiki wa Simba kumuunga mkono na kumuamini Mpanzu katika kipindi hiki kigumu, akisisitiza kuwa mshikamano ndio nguzo muhimu ya mafanikio ya timu.

The post SIMBA KUMLINDA MPANZU, KINACHOMTESA AHMED AFICHUA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA YAMUACHA MDOMO WAZI KOCHA STADE MALIEN
Next Post BUBA PULIZA MOTO YANGA, JINA LAKIMBIWA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook