Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MABADILIKO YA BENCHI YALIVURUGA SIMBA, MANGUNGU

  • 33
Scroll Down To Discover

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, amesema mabadiliko ya ghafla katika benchi la ufundi yamechangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu kwa timu hiyo.

Mangungu amesema msimu uliopita Simba ilikuwa chini ya kocha mpya, Fadlu Davids, ambaye alihitaji aina maalumu ya wachezaji watakaokwenda sambamba na falsafa yake ya soka, jambo lililowasaidia kumaliza msimu katika nafasi ya pili na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ameeleza kuwa walipoanza msimu huu, uongozi uliingia sokoni kusajili wachezaji kulingana na mapendekezo ya kocha huyo, lakini ujio wa ofa kubwa kwa Davids uliwalazimu kumuacha aondoke, hali iliyovuruga mipango yao mapema.

“Wakati tunaanza msimu na kusajili wachezaji aliowapendekeza, ikaja ofa kubwa kwake na hatukuwa na budi kumzuia. Hilo lilituvuruga sana kwa sababu tulilazimika kuingia sokoni tena kutafuta kocha mwingine,” amesema Mangungu.

Ameongeza kuwa Simba ilifanikiwa kumpata Steve Barker, ambaye naye amekuja na falsafa yake ya uchezaji, hivyo kulikuwa na ulazima wa kufanya usajili mwingine wa wachezaji watakaosaidia timu kufikia malengo yake.

Mangungu amesema ujio wa kocha mpya katikati ya mashindano, pamoja na usajili wa wachezaji wapya, bado ni changamoto kwa timu kutokana na kukosekana kwa muunganiko wa pamoja.

Amefafanua kuwa mafanikio ya timu si juhudi zake peke yake bali ni matokeo ya ushirikiano wa viongozi wengine, hata hivyo lawama nyingi hutupwa kwake pale timu inapofanya vibaya.

“Jambo ninalokubaliana nalo ni waache wapewe sifa wanaowapenda, lakini lawama zije kwangu. Mimi siwezi kufanya timu ifanye vibaya kwa makusudi, kwa sababu tumeunda bodi na menejimenti yenye uwezo wa kufanya kazi na benchi la ufundi au wachezaji,” amesema.

Ameongeza kuwa kulingana na mgawanyo wa majukumu, yeye binafsi hana nafasi ya kukutana moja kwa moja na wachezaji, bali bodi hukaa na kuwasilisha maelekezo kwa menejimenti ili yawafikie wachezaji.

Mangungu amesema kelele na vurugu zinazoshuhudiwa hazichochewi na mashabiki au wanachama wa kweli wa Simba, bali ni watu wachache walioundwa kwa ajili ya propaganda na kuiondoa klabu hiyo kwenye mstari wake.

The post MABADILIKO YA BENCHI YALIVURUGA SIMBA, MANGUNGU appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA TUPAMBANE KULINDA HESHIMA YETU, BARKER
Next Post YANGA KUSAKA POINTI MOROCCO
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook