Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

JOTO LAWAKUTANISHA AL AHLY AMANI

  • 43
Scroll Down To Discover

Mapema tu leo Al Ahly imeonyesha kuanza kutishwa na hali ya joto kwenye Uwanja wa New Amaan Complex mjini Unguja ikisaka maji kwa haraka kabla ya kuanza kwa mazoezi.

Timu hiyo ambayo kesho itakuwa mgeni wa Yanga kwenye mchezo wa nne wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, imetua Uwanja Amaan saa 9:55 tayari kwa mazoezi ya mwisho ambapo mara baada makocha kuzigusa nyasi wakaomba umwagiwe maji haraka.

Maofisa wa Al Ahly wameonekana wakiwahimiza wasimamizi wa Uwanja wa Amaan kufungulia mabomba haraka kabla ya kuanza kwa mazoezi hayo.

Kocha Jesse Thorup ameonekana akiwarudisha wachezaji wake vyumbani akiwaambia joto ni kali uwanjani na wataitwa baada ya mabomba kufunguliwa.

Dakika chache baadaye baada ya mabomba hayo kufunguliwa timu hiyo ikaendelea na ratiba ya mazoezi kwenye uwanja huo.

Wakati Ahly ikianza mazoezi ikapishana na waamuzi wa mchezo huo kutoka Cameroon ambapo maofisa wa juu wa klabu hiyo wamesikika wakisisitiza kwamba dakika za mapumziko kunywa maji (water break) wakiomba yazingatiwe kutokana na hali ya joto.

Leo, hali ya hewa Zanzibar inasoma nyuzi joto 31 ambapo Al Ahly imeonyesha wasiwasi wa wachezaji kukabiliana nayo.

The post JOTO LAWAKUTANISHA AL AHLY AMANI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post ALIYEINYONGA AZAM KUCHEZESHA YANGA NA AL AHLY
Next Post Marekani, Israel Zakanusha Kuhusika na Milipuko Iran – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook