Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yateua Mbunge na Diwani wa Viti Maalumu

  • 40
Scroll Down To Discover

Beng’i Mazana Issa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Viti Maalumu.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake kilichofanyika leo Januari 30, 2026 imefanya uteuzi wa Ndugu. Beng’i Mazana Issa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Halima Idd Nassor, wa CCM aliyefariki tarehe 18 Januri 2026.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi waTume hiyo, Kailima Ramadhani, imesema uteuzi huo wa Beng’i Issa, umezingatia masharti ya Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 112 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani, Sura ya 343,

Aidha, taarifa hiyo imesema kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 25(1)(c) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288 kikisomwa pamoja na kifungu cha 113 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343, Tume katika kikao hicho imefanya uteuzi wa Ndugu Irene Linus Mwangara wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kuwa Diwani wa Viti Maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Uteuzi huo umefanyika baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa marudio katika kata ya Mzinga, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo uchaguzi uliahirishwa kutokana na kifo cha mgombea katika kata husika.

 

The post Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yateua Mbunge na Diwani wa Viti Maalumu appeared first on Global Publishers.



Prev Post Afrika Kusini Yamfukuza Balozi wa Israel, Yampa Saa 72 Kuondoka
Next Post Rais Dkt. Mwinyi: Mwezi Wa Ramadhan Si Kisingizio Cha Kupanda Kwa Bei Za Bidhaa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook