Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TUTAFURAHI MECHI YA NYUMBANI, TSHABALALA

  • 44
Scroll Down To Discover

BEKI wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema kikosi cha timu hiyo kimejipanga kuhakikisha kinawapa furaha mashabiki wao katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Yanga itakuwa nyumbani Januari 31, 2026, katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa kwenye dimba la New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya kikosi hicho, Tshabalala amesema wamejifunza kutokana na makosa yaliyotokea katika mchezo wa kwanza na sasa wanarejea nyumbani wakiwa na lengo la kusawazisha makosa na kupambana kwa nguvu zote.

Amesema  licha ya ugumu wa mchezo uliopita, wachezaji walitekeleza maelekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Pedro Goncalves, lakini matokeo hayakuwa yale waliyotarajia.

“Huu ulikuwa mchezo mgumu, tulisimama vizuri katika mipango ya mwalimu, lakini hatukupata matokeo tuliyoyahitaji,” amesema  Tshabalala.

Ameongeza kuwa hatua ya makundi ni ndefu na bado kuna nafasi ya kurekebisha hali, huku akiahidi kuwa katika mchezo wa nyumbani watahakikisha wanaibuka na matokeo chanya.

“Hizi ni mechi za makundi, ni marathon. Kuna mchezo mwingine wa marudiano nyumbani dhidi yao, tutahakikisha tunapambana na sisi tunafurahi vizuri,” amesema  Tshabalala.

The post TUTAFURAHI MECHI YA NYUMBANI, TSHABALALA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA YAWEKA WAZI SABABU YA KUKOSA MAZOEZI
Next Post PEDRO AJIVUNIA YANGA LICHA YA KIPIGO MISRI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook