Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

YANGA YAJIPANGA NA MIPANGO HATARI

  • 45
Scroll Down To Discover

OFISA Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kikosi cha timu hiyo kimemaliza salama mchezo wao dhidi ya Al Ahly bila kupata majeruhi wowote, jambo ambalo ni faraja kubwa kwa benchi la ufundi kuelekea michezo ijayo ya hatua ya makundi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kamwe amesema Al Ahly wamefanikiwa kupata matokeo mazuri wakiwa nyumbani kwao, huku wakikiri kuwa timu hiyo imekuwa ikipata changamoto inapocheza mechi za ugenini katika mashindano hayo.

Ameeleza kuwa hatua ya makundi ni ngumu na inahitaji hesabu kubwa, huku kila timu ikipambana kuhakikisha inakusanya pointi muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kamwe amesema ushindi wa Al Ahly ni jambo la kawaida kwao wanapocheza nyumbani, na amesisitiza kuwa Yanga haina sababu ya kukata tamaa kwani bado nafasi ya kufanya vizuri ipo wazi.

Ameongeza kuwa Yanga nayo ina kila sababu ya kufurahi itakapocheza nyumbani Januari 31, ambapo mashabiki wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kuipa timu hiyo sapoti kubwa katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu.

“Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tunaenda kujipanga vizuri ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri nyumbani. Tuna imani na kikosi chetu,” amesema Kamwe.

The post YANGA YAJIPANGA NA MIPANGO HATARI appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA BADO NAFASI YA DHAHABU MAKUNDINI
Next Post SIMBA YAWEKA WAZI SABABU YA KUKOSA MAZOEZI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook