Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbowe Aitaka Serikali Kuwaachia Wafungwa wa Kisiasa Ili Kuponya Taifa – Video

  • 32
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ameitaka Serikali kukiri ukweli na kuwaachia wafungwa wa kisiasa waliopo magerezani ili kuponya majeraha ya watanzania ambao wana maumivu makubwa.

Akizungumza wakati wa salamu fupi za familia katika ibada ya mazishi ya Mzee Mtei, Mbowe amewataka Waziri Mkuu pamoja na viongozi wengine wa serikali kutambua kuwa taifa bado lina maumivu makubwa.

“Nitakuwa mnafiki nisipolisema hili. Maendeleo mnayoniambia serikali inasimamia ni jambo jema, lakini hakuna jambo la maana na la muhimu kuliko uhuru wa watu katika nchi yao,” amesema Mbowe.

Ameongeza kuwa viongozi wa CHADEMA waliopo magerezani wanaendelea kuumiza mioyo ya Watanzania, akisisitiza kuwa magereza yamejaa viongozi wa kisiasa ambao walipaswa kuwa huru, uraiani, wakishiriki na kuona matunda ya nchi yao.
“Njia bora ni kurejesha uhuru wa watu, haki za watu, na serikali ikiri ukweli pale ilipokosea,” amesisitiza Mbowe.

Aidha, amesema kuwa kwa jinsi anavyomfahamu marehemu Mzee Edwin Mtei, alikuwa ni mtu mwenye misimamo thabiti, asiyeyumba na aliyekuwa akitekeleza kwa vitendo ahadi alizoamini.

The post Mbowe Aitaka Serikali Kuwaachia Wafungwa wa Kisiasa Ili Kuponya Taifa – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post AHOUA AAGANA NA SIMBA, ATUA CR BELOUIZDAD
Next Post Dkt. Mwigulu Atoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa Mzee Edwin Mtei
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook