Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

AFCON Yazua Balaa: Gabon Yasimamisha Timu, Aubameyang Afungiwa na Kocha Atimuliwa!

  • 26
Scroll Down To Discover

Serikali ya Gabon imesitisha ushiriki wa timu ya taifa ya soka “The Panthers” na kumfungia mshambuliaji nyota Pierre-Emerick Aubameyang, kufuatia kutolewa kwao kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Hatua hizo zilitangazwa na Waziri wa Michezo, Simplice-Desire Mamboula, baada ya Gabon kufungwa 3–2 na Ivory Coast mnamo Desemba 31, huku wakimaliza mkiani katika kundi lao nchini Morocco baada ya pia kupoteza dhidi ya Cameroon na Mozambique.

Mamboula alieleza kuwa serikali imeamua:

  • Kuvunja benchi la ufundi,

  • Kusimamisha timu ya taifa hadi taarifa nyingine,

  • Kuwafungia Bruno Ecuele Manga na Pierre-Emerick Aubameyang.

Alisema matokeo hayo yalikuwa “aibu” kwa taifa, licha ya Gabon kuanza mechi ya mwisho kwa kuongoza mabao mawili kabla ya kupoteza mchezo.

Aubameyang, aliyewahi kuchezea Arsenal na Chelsea, hakucheza mechi ya mwisho baada ya kurejea Marseille kwa matibabu ya jeraha la paja, akisisitiza kuwa changamoto ndani ya timu “ni kubwa kuliko mchezaji mmoja”.

Kocha Thierry Mouyouma, aliyekuwa kwa zaidi ya miaka miwili, pia ametimuliwa. Serikali nyingi barani Afrika kuchukua hatua kama hizi, matukio ya aina hiyo yamepungua kutokana na msimamo mkali wa Fifa dhidi ya kuingiliwa kwa masuala ya soka na serikali.

KIJANA ALIYEFANYA KAZI za ULINZI ASIMULIA MSOTO HADI KUANZISHA BIASHARA ya MAMILIONI – AAJIRI WATU

The post AFCON Yazua Balaa: Gabon Yasimamisha Timu, Aubameyang Afungiwa na Kocha Atimuliwa! appeared first on Global Publishers.



Prev Post TRA Yavunja Rekodi, Oktoba hadi Desemba Yakusanya Sh. Trilioni 9
Next Post Watu 40 Wafariki, Zaidi ya 100 Wajeruhiwa Mkesha wa Mwaka Mpya – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook