Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TRA Yakamata Madumu 23,755 Ya Mafuta Ya Kupikia Ya Magendo Dar – Video

  • 49
Scroll Down To Discover

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo imekamata Shehena kubwa ya Mafuta ya kupikia ya Magendo, jumla ya Madumu 23,755, yaliyokuwa yakiingizwa nchini kinyume na taratibu kupitia Bandari ya Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, akizungumza mara baada ya zoezi hilo, amesema kuwa bidhaa hizo za Magendo zimekuwa tishio kwa Uchumi wa nchi, kwa kuwa zinapunguza Mapato ya Serikali na kudhoofisha ukuaji wa Viwanda vya ndani.

Aidha, aliongeza kuwa bidhaa hizo zisizopitia ukaguzi wa Mamlaka husika huweza kuwa hatari kwa afya za walaji, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki katika kuzuia biashara hiyo haramu.

TRA imesisitiza kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wa Biashara za Magendo, huku ikihamasisha Wananchi kushirikiana katika kutoa taarifa ili kulinda Uchumi wa Taifa.

The post TRA Yakamata Madumu 23,755 Ya Mafuta Ya Kupikia Ya Magendo Dar – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mahakama Kuu Yakataa Pingamizi, Kesi ya Uchaguzi Kigoma Mjini Kuendelea
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 18, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook