Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Mwigulu Ashiriki Mazishi Ya Jenista Mhagama, Atoa Maagizo Kwa Mkandarasi Wa Barabara Ya Kitai–Ruanda (Picha +Video)

  • 47
Scroll Down To Discover


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Desemba 16, 2025 ameshiriki katika Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma

Akizungumza katika mazishi hayo, Dkt. Mwigulu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kumsimamia mkandarasi anayejenga barabara ya Kitai hadi Ruanda ili akamilishe ujenzi wa barabara hiyo muhimu kwa wakazi wa mkoa huo.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema tayari Serikali ilikwisha kutoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo kwa kutambua umuhimu wake kwenye uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

“Ni dhahiri kabisa kwamba kasi ya ujenzi hairidhishi nikutake mkuu wa mkoa, mwite mkandarasi huyu mara baada ya shughuli hii, mwambie alishapokea fedha sasa afanye kazi ionekane, kama ameshatumia pesa hiyo kwenye kazi nyingine kamata passport yake asitoke mpaka kazi hii ikamilike”

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi aliwaongoza waombolezaji kwenye mazishi hayo.

The post Dkt. Mwigulu Ashiriki Mazishi Ya Jenista Mhagama, Atoa Maagizo Kwa Mkandarasi Wa Barabara Ya Kitai–Ruanda (Picha +Video) appeared first on Global Publishers.



Prev Post Makamu wa Rais Nchimbi Aongoza Mazishi ya Jenista Mhagama Ruanda – Mbinga (Picha +Video)
Next Post Makamu wa Rais Aitaka Kampasi ya UDSM Kagera Kukuza Ujuzi na Ujasiriamali wa Vijana
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook