NA DENIS MLOWE, IRINGA
MSANII wa muziki wa bongo fleva kutoka mkoani Iringa na DJ maarufu Nickson Sanga maarufu kama Dj Nass anatarajiwa kufanya tamasha kubwa la kila mwaka linalojulikana kama ‘Friend of DJ Nass’ litakalojumuisha burudani pamoja na kugusa maisha ya jamii kwa vitendo.
Akizungumza na wanahabari mkoani hapa, Dj Nass alisema kuwa Kabla ya tamasha hilo, kutakuwa na zoezi maalum la kutoa msaada kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika Kituo cha Nyumbahali, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo na mshikamano kwa jamii.
Alisema kuwa Wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi wakiwa na vitu mbalimbali vya msaada kama vile nguo, vyakula, vifaa vya shule na mahitaji mengine muhimu ili kuweza kutoa msaada huo kwa kituo hicho.
Katika tukio hilo la kijamii, Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James, jambo linaloonesha uzito na umuhimu wa tukio hili kwa jamii.
Baada ya zoezi la kutoa msaada, burudani itaendelea kwa tamasha kubwa litakalofanyika katika Ukumbi wa Backyard Lounge. Wasanii mbalimbali watatoa burudani kali akiwemo:msanii mkongwe Dully Sykes ambaye wataambatana na B2K na Lony Bway.
Tamasha hili linatarajiwa kuwa jukwaa la kuunganisha burudani, upendo na mshikamano wa kijamii na kutoa wito kwa watu maarufu kuwa na utaratibu wa kuwakumbuka wenye uhitaji.
Wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi kushiriki, kusaidia jamii na kufurahia burudani ya kipekee ambapo tamasha hilo litafanyika Disemba 19 mwaka huu.











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!