Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

AGNESS SULEIMAN KAHAMBA (AGGYBABY ) ASHINDA TUZO YA MWIGIZAJI BORA WA KIKE WA TANZANIA MWAKA 2025 

  • 8
Scroll Down To Discover

Msanii wa Muziki na Maigizo Bi Agness Suleiman Kahamba maarufu kama (Aggybaby) amepokea Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike wa Mwaka 2025 kutoka Achievers Awards International ya nchini Nigeria kutokana na kazi zake za sanaa ya uigizaji na shughuli zake za huduma kwa jamii kupitia taasisi yake—Tupaze Sauti Foundation (Tanzania). 

Waandaaji wa tuzo hizi wametambua kazi nzuri anayoifanya mwanatasnia Agness katika sekta ya filamu hususani kupitia tamthiliya za “Panguso”, “Huba” na kazi zake nyingine za filamu katika mtandao wa YouTube. 

Tuzo hii ni alama ya ushirikiano wa kifilamu uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Nigeria .Bi Agness amebainisha kwamba waandaaji wa tuzo hizi wanavutiwa sana na filamu kutoka Tanzania kipekee wautaja utamaduni wetu, amani na ushirikiano unaooneshwa katika filamu zetu kuwa alama ya utu wa mwafrika—akinasibisha yale wanayoyaona kupitia tamthiliya ya “Kombolela”.

Leo, Jumatatu Tarehe 13 Oktoba 2025—Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga (PhD) amekutana na kufanya mazungumzo na mwatasania wa filamu na michezo ya kuigiza nchini—Agness Suleiman Kahamba @aggybaby__

Pia Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Gervas Kasiga (PhD) amempongeza Agness kwa juhudi zake za kufanya kazi bora za filamu na kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika majukwaa ya filamu kimataifa. 

Aidha, Dkt. Kasiga (PhD) amemsihi Agness kuendelea kufanya kazi zake za sanaa kwa ubunifu na weledi mkubwa ili kuutangaza vyema utamaduni wetu wa Kitanzania ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.



Prev Post Tanzania Yashiriki Kongamano la Afya Duniani Jijini Berlin
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO OKTOBA 14, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook