Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Katibu wa Bunge Aeleza Chanzo cha Kifo cha Jenista Mhagama – Video

  • 24
Scroll Down To Discover

Chanzo cha kifo cha aliyekuwa Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Joakim Mhagama, kimetajwa kuwa ni maradhi ya moyo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 13, 2025 na Katibu wa Bunge, Baraka Leonard, wakati akisoma wasifu wa marehemu katika misa takatifu ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jenista Mhagama, iliyofanyika jijini Dodoma, mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi wengine wa kitaifa.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, marehemu alifariki dunia Desemba 11, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini Dodoma.

Katika wasifu wake, marehemu Jenista Mhagama ametajwa kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika sekta ya afya, Bunge na maendeleo ya jamii, akitumikia Taifa kwa uadilifu na kujitolea hadi mwisho wa maisha yake.

Ibada hiyo ya kuaga imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, wabunge, viongozi wa dini, wanafamilia, pamoja na waombolezaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi, huku Taifa likiendelea kuomboleza msiba huo mkubwa.

The post Katibu wa Bunge Aeleza Chanzo cha Kifo cha Jenista Mhagama – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Usikose! Ajira 514 Zatangazwa Afya, TEHAMA na Ufundi – Deadline Disemba 23
Next Post Mwili wa Marehemu Jenista Mhagama Waagwa Dodoma, Mazishi Desemba 16 Peramiho – (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook