Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wananchi Dar ‘Walia’ na Tatizo la Maji, Wadai Bili Zinaendelea Kuwafika Bila Huduma

  • 67
Scroll Down To Discover

Wananchi wa Dar es Salaam wameendelea kuonesha malalamiko yao kutokana na ukosefu wa maji safi katika maeneo mbalimbali ya jiji, hali ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa maisha ya kila siku. Tatizo hili limeathiri matumizi ya nyumbani, shule, na biashara ndogo ndogo, huku familia nyingi zikikosa maji.

Wakazi wamesema wanashangazwa na kuendelea kupokea bili za maji kila mwezi, licha ya huduma hiyo kutowafikia.

Miongoni mwa maeneo yenye tatizo kubwa ni Tabata, Kisukulu, Kwa Mkua, Makoka Shule ya Msingi, Ubungo, Sinza, Mwenge Mpakani, pamoja na maeneo mengine yanayozunguka jiji.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, hivi karibuni alisisitiza kwamba huduma ya maji itatolewa kwa mgao na kwa usawa, kuhakikisha kila sehemu ya Dar es Salaam inapata huduma hii muhimu. Hata hivyo, baadhi ya wananchi bado hawajapata maji, jambo ambalo limeendelea kuwa changamoto katika mwezi wa pili mfululizo.

Wananchi wanaiomba Wizara ya Maji na mamlaka husika kuhakikisha usambazaji wa maji unakuwa wa haki, endelevu, na unafikiwa kwa wakati ili kuondoa usumbufu unaokumba familia na biashara ndogo ndogo.

TAARIFA NZITO ya JESHI la POLISI LEO – LATANGAZA HALI ya USALAMA NCHINI – “TANZANIA IMETULIA”..

The post Wananchi Dar ‘Walia’ na Tatizo la Maji, Wadai Bili Zinaendelea Kuwafika Bila Huduma appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu wa Bulgaria Ajiuzulu Baada ya Maandamano Makubwa
Next Post Tambua Setingi Muhimu Kwenye Simu Yako ya Android Ili Kujilinda
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook