Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Tasnia ya Filamu Yapoteza Mwigizaji Laisa, Msiba Wathibitishwa – Video

  • 66
Scroll Down To Discover

Tasnia ya filamu nchini imepokea taarifa za msiba wa Laisa, ambaye alikuwa mfanyabiashara na muigizaji katika BongoMuvi. Taarifa hizo sasa zimethibitishwa rasmi baada ya mazungumzo na mfanyabiashara na mtu wa karibu wa marehemu, @sophie_amelowa, ambaye amekiri kuwa msiba huo umetokea leo.

Kwa mujibu wa Sophie, tasnia imepoteza kijana aliyekuwa na juhudi, mipango, na malengo mengi ndani ya sanaa na biashara. Amesema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwa wale waliomfahamu na kushirikiana naye.

Chanzo cha Kifo

Chanzo cha kifo cha Laisa kinatajwa kuhusishwa na tatizo la presha pamoja na msongo wa mawazo, ingawa taarifa za matibabu kutoka kwa madaktari bado hazijatolewa rasmi. Familia na watu wa karibu wanatoa wito kwa umma kusubiri taarifa sahihi zaidi kutoka kwa wahudumu wa afya na ndugu.

The post Tasnia ya Filamu Yapoteza Mwigizaji Laisa, Msiba Wathibitishwa – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Video: Polisi Watoa Ufafanuzi Kuhusu Kukamatwa Kwa Geofrey Mwambe
Next Post Waziri Mkuu wa Bulgaria Ajiuzulu Baada ya Maandamano Makubwa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook