Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbunge Jenista Mhagama, Afariki Dunia Leo, Dodoma

  • 58
Scroll Down To Discover

Aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama.

Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, amefariki dunia leo 11 Desemba 2025 jijini Dodoma. Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, ambaye amesema kuwa Bunge limepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa.

Spika Zungu ametuma salamu za pole kwa Wabunge, familia, ndugu, jamaa, pamoja na wananchi wa Jimbo la Peramiho. Aidha, amewaomba Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge zinaonyesha kuwa mpango wa mazishi ya Jenista Mhagama utatolewa kwa kushirikiana na familia yake, huku mashabiki na wananchi wakitarajia kuwa na nafasi ya kumkumbuka na kumzika kwa heshima zinazostahili kiongozi wa taifa.

The post Mbunge Jenista Mhagama, Afariki Dunia Leo, Dodoma appeared first on Global Publishers.



Prev Post CEOrt na IUCN Waunganisha Nguvu Kuleta Mapinduzi ya Kijani Sekta ya Utalii
Next Post Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatangaza Siku 10 za Mvua
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook