Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Chalamila: Msipotoshwe, Hali ya Usalama Iko Vizuri Jijini Dar – Video

  • 37
Scroll Down To Discover


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amezungumza na Global TV akitoa tathmini ya hali ya ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam, ambapo amesema jiji lipo katika utulivu na shughuli za wananchi zinaendelea kama kawaida.

Katika mahojiano hayo, Chalamila ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea na doria na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha hakuna vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani. Amesisitiza kuwa wananchi waendelee kuwa watulivu na kufanya shughuli zao bila hofu.

Aidha, Chalamila ametoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu ambao, kwa maneno yake, “hawakuelewa ipasavyo” maelezo ya Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, yaliyotolewa hivi karibuni. Amesema kauli ya Waziri Mkuu ilikuwa ya kuhimiza utulivu na kufikisha ujumbe wa Serikali kuhusu kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani.

Ameongeza kuwa ni muhimu Watanzania kusoma na kusikiliza taarifa za Serikali kwa usahihi, badala ya kutegemea tafsiri potofu zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Chalamila amehitimisha kwa kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali na vyombo vya ulinzi katika kulinda amani ya jiji na nchi kwa ujumla.

The post Chalamila: Msipotoshwe, Hali ya Usalama Iko Vizuri Jijini Dar – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Simbachawene Awapongeza Askari kwa Kulinda Amani Kufuatia Fununu za Maandamano – Video
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 10, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook