Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Polisi Watoa Taarifa Kuhusu Hali ya Usalama Asubuhi ya Leo – Video

  • 54
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi limetoa taarifa rasmi kwa umma leo Jumatano, Desemba 10, 2025, likielezea hali ya ulinzi na usalama nchini katika saa za asubuhi.

Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kuwa hali ya usalama imeendelea kuwa shwari katika maeneo yote, huku askari wakiendelea kufanya doria na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao bila wasiwasi.

Polisi wamesisitiza kuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yenye msongamano wa watu, barabara kuu na mitaa ya mijini, ikiwa ni sehemu ya hatua za kutuliza hofu kufuatia taarifa na fununu mbalimbali zilizokuwa zikisambaa mtandaoni.

Aidha, Jeshi la Polisi limewahimiza wananchi kuendelea kuwa watulivu na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani.

The post Polisi Watoa Taarifa Kuhusu Hali ya Usalama Asubuhi ya Leo – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Trump Atoa Shinikizo Kwa Zelensky Kuhusu Makubaliano ya Amani
Next Post Waziri Simbachawene Awapongeza Askari kwa Kulinda Amani Kufuatia Fununu za Maandamano – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook