Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Watoto 100 wa Shule Watachiliwa Huru Jimbo la Niger, Nigeria

  • 67
Scroll Down To Discover

Serikali ya Nigeria imefanikisha kuachiliwa huru watoto 100 wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita katika Jimbo la Niger. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya Channels Television.

Hata hivyo Channels Television haikutoa maelezo zaidi kuhusu namna wanafunzi hao walivyoachiliwa.
Chama cha Wakristo cha Nigeria kilitangaza hapo kabla kuwa watoto 303 na wafanyakazi 12 wa shule walitekwa nyara Novemba 21 mwaka huu na watu wenye silaha katika shule ya Dakhalia ya Kanisa Katoliki ya St Mary’s huko Papiri.

Wanafunzi 50 walifanikiwa kutoroka katika saa zilizofuata, lakini tangu wakati huo hakujakuwa na taarifa kuhusu waliko au hali za watoto wengine. Imeelezwa kuwa baadhi yao walikuwa na umri wa miaka sita tu.
Ikulu ya Rais wa Nigeria kupitia msemaji wake Sunday Dare imethibitisha kuachiliwa baadhi ya wanafunzi waliokuwa wametekwa nyara.

Aidha, chanzo kimoja kimevieleza vyombo vya habari kwamba waathirika walioachiliwa “watakabidhiwa kwa serikali ya Jimbo la Niger leo Jumatatu”.

Shambulio dhidi ya shule jimboni Niger lilidhihirisha ukosefu wa usalama nchini Nigeria, ikiwa imepita zaidi ya miaka 10 tangu ulipotokea utekaji nyara wa wasichana wanaokaribia 300 kwenye mji wa Chibok ulioko kusini mwa jimbo la Borno kaskazini mashariki ya nchi hiyo.

The post Watoto 100 wa Shule Watachiliwa Huru Jimbo la Niger, Nigeria appeared first on Global Publishers.



Prev Post MATESO YA GAMONDI YANAMTESA PEDRO KWA YANGA
Next Post Zelenskyy Asema Yuko Tayari Kuandaa Uchaguzi wa Rais Hata Wakati wa Vita
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook