Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Video: PM Mwigulu Awasilisha Ujumbe wa Rais Samia Kuhusu Sikukuu ya Uhuru

  • 65
Scroll Down To Discover

Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasilisha rasmi ujumbe wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuelekea maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru yatakayofanyika kesho, Jumapili Desemba 09, 2025.

Amesema kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya Rais, kesho itakuwa siku ya mapumziko ya kitaifa, hivyo Watanzania wanashauriwa kutulia majumbani na kuitumia siku hiyo kwa kutafakari historia, thamani, na tunu za uhuru wa taifa.

Waziri Mkuu amebainisha kuwa ni muhimu wananchi kuitumia siku hiyo kujenga umoja, kuenzi amani na kuendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa wale ambao majukumu yao ya kikazi yanawalazimu kutoka, kama huduma muhimu kwa umma, wataendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida.

Amehitimisha kwa kuwatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya Uhuru na kuwasihi kuendelea kudumisha utulivu, mshikamano na uzalendo.

The post Video: PM Mwigulu Awasilisha Ujumbe wa Rais Samia Kuhusu Sikukuu ya Uhuru appeared first on Global Publishers.



Prev Post Simbachawene Awapa Polisi Maagizo Mapya ya Kukamata Watuhumiwa – Video
Next Post Fahamu Maajabu ya Mbuga ya Taifa ya Serengeti, Tanzania
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook