Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mbunge Mstaafu na Naibu Waziri Benedict Ole Nangoro Afariki Dunia

  • 82
Scroll Down To Discover

 

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne, na Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Benedict Ole Nangoro.

Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne, na Mbunge mstaafu wa Jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Benedict Ole Nangoro, amefariki dunia leo Desemba 7, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Arusha.

Msemaji wa familia, Christopher Ole Sendeka, amesema Ole Nangoro alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo, na aliwahi kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma pamoja na hospitali nchini Kenya.

Amesema kwa sasa familia inaendelea na maandalizi, ikiwemo kupanga tarehe ya mazishi na eneo atakapozikwa.

MUFTI BAKWATA ATOA KAULI KUHUSU TEC na MAUAJI OKT 29 – ”NI HARAMU KUIUA NAFSI YA MTU BILA HAKI…”

The post Mbunge Mstaafu na Naibu Waziri Benedict Ole Nangoro Afariki Dunia appeared first on Global Publishers.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 07; 2025
Next Post Sheikh Mkuu wa Tanzania Awataka Watanzania Kuendeleza Uchumi Bila Kuvuruga Amani – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook