Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KUELEKEA AFCON 25…..53 WA TAIFA STARS HAWA HAPA…..PANGA LA MWISHO MHHHH….

  • 83
Scroll Down To Discover

KOCHA Mkuu wa Taifa Stars Miguel Gamondi ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 53 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21 mwaka huu hadi Januari 18, mwakani.

Kikosi hicho kina wachezaji wakongwe na wazoefu wa michuano hiyo wakiongozwa na Mbwana Samatta na Simon Msuva. Pia, kina wachezaji chipukizi na wengine waliwahi kuitwa kwa vipindi tofauti.

Tanzania ipo Kundi C kwenye michuano hiyo ya AFCON 2025 sambamba na Nigeria, Tunisia na Uganda ambapo Stars inatarajia kuondoka nchini Desemba 8, mwaka huu kwenda nchini Misri kuweka kambi ya maandalizi ya michuano hiyo.

Walioitwa ni pamoja na Hussein Masalanga, Mukrim Abdallah, Khalid Habibu, Nickson Kibabage wote (Singida Black Stars) Yakoub Suleiman, Morice Abraham, Wilson Nangu, Yusuph Kagoma, Shomari Kapombe , Vedastus Masinde, Suleiman Mwalimu na Kibu Dennis (Simba SC).

Kelvin Nashon, Yona Amos (Pamba Jiji FC), Zuberi Foba, Iddi Suleiman, Nassor Saadun, Nathaniel Chilambo, Lusajo Mwaikenda, Yahya Zaydi, Pascal Msindo, Elias Lawi, Abdul Suleiman, Feisal Salum ‘Feitoto’ (Azam FC), Haji Mnoga (Salford City, England), Ibrahim Abdulla, Dickson Job, Mohamed Hussein, Mudathir Yahya, Offen Chikola, Bakari Mwamnyeto, Israel Mwenda (Yanga).

Cyprian Kachwele (Whitecaps Fc, Canada), Ahmed Pipino (KMC FC), Mbwana Samatta (Le Havre, Ufaransa), Simon Msuva (Al-Talaba Sc, Iraq), Athumani Makambo (Coastal Union), Novatus Miroshi (Göztepe Fc, Turkey), Tarryn Allarakhia (Rochdale, England), Charles M’mombwa (Floriana FC, Malta).

Iddi Kipagwile (Dodoma Jiji), Vitalisy Mayanga (Mbeya City), Edwin Balua (En Paralimniou, Cyprus), Miano Danilo (FK, Panevezys, Lithuana)

Alphonse Mabula (FC Shamakhi, Azerbaijan), Abdukarim Kiswanya (Namungo FC), AbdulMalik Zakaria (Mashujaa FC), Said Khamis (Immigration FC, Malaysia), Jackson Kasanzu (Tomenta FC, USA)

Kelvin John (Aalborg BK, Denmark), Sabri Kondo (BK Hacken, Sweden), Paul Peter (JKT Tanzania) na Abel Josiah (JKT Tanzania U20).

The post KUELEKEA AFCON 25…..53 WA TAIFA STARS HAWA HAPA…..PANGA LA MWISHO MHHHH…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BAADA YA KUFUNGA GOLI 1 LA LIGI….BAJABER AFUNGUKA MAGUMU YA SIMBA…
Next Post AUCHO KWENYE RADA ZA KOCHA WA SIMBA…OFA NONO YAWEKWA MEZANI….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook