Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Spika Zungu Aonana na Mabalozi wa EU, Mazungumzo Yalenga Kuimarisha Ushirikiano wa Kibunge

  • 57
Scroll Down To Discover

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU),  Christine Grau walipomtembelea leo tarehe 4 Desemba, 2025 katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha diplomasia ya kibunge (Parliamentary Diplomacy).

Kikao hicho kimehudhuria na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Balozi wa Finland, Balozi wa Hispania, Balozi wa Italia, Balozi wa Ubelgiji na Balozi wa Ujerumani.

The post Spika Zungu Aonana na Mabalozi wa EU, Mazungumzo Yalenga Kuimarisha Ushirikiano wa Kibunge appeared first on Global Publishers.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO DISEMBA 04, 2025
Next Post RC Arusha Awakilisha Tanzania Katika Maandalizi ya Mkutano wa Mabunge Duniani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook