Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jeshi la Polisi: Gwajima, Mnyika, Lema na Wengine Watajwa Kwenye Orodha ya Wanaosakwa

  • 16
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Nchini limeutangazia umma wa Watanzania kuwa kufuatia matukio ya vurugu, uporaji wa mali na uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29.2025 katika Majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, na pia katika mikoa ya Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara Dodoma, Kilimanjaro na Iringa ambazo zimesababisha madhara kwa binadamu, kuharibu mali nyingi za umma na za watu binafsi kumeleta athari kubwa

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo Novemba 07.2025 imeeleza kuwa mbali na athari kwa uhai na maisha ya watu, waliofanya uhalifu huo pia wameharibu na kuchoma moto mali za umma kama vile Ofisi za TRA, TAKUKURU, Mahakama, ATM za baadhi ya Benki, Vituo vya Polisi, Vituo vya Mabasi ya Mwendokasi kutoka Kimara mwisho hadi Magomeni na kutoka Magomeni hadi Morocco, Ofisi za Serikali za Mitaa, kuchoma moto barabara za lami na za zege kwa kutumia matairi na majengo kadhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Aidha Jeshi laPolisi limeendelea kueleza kuwa, baadhi ya mali za watu binafsi zimeharibiwa na kuchomwa moto kama vile Vituo vya mafuta, Maduka mbalimbali, Magari makubwa na madogo, pia wamehusika wamefanya uporaji wa mali na pesa za watu kutoka maeneo mbalimbali ya biashara

“Pamoja na kwamba baadhi ya waliopanga kutekeleza uhalifu huo wamekamatwa na kuanza kufikishwa Mahakamani, Jeshi la Polisi Nchini kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta wale wote waliopanga, kuratibu na kutekeleza uovu huo, aidha wakati hatua hizo zikiendelea, jamii inaombwa kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika kutoa taarifa za watu wote waliohusika ili hatua sahihi za kisheria zichukuliwe dhidi yao” -Jeshi la Polisi

Kupitia taarifa hiyo pia, Jeshi hilo limesema kufuatia uchunguzi na ushahidi uliokusanywa hadi sasa linawasaka kwaajili ya kuwakamata Josephat Gwajima, Brenda Jonas Rupia, John Mnyika, Godbless Jonathan Lema, Machumu Maximilian Kadutu, Deogratias Cosmas Mahinyila, Boniface Jacob, Hilda Newton, Award Kalonga na Aman Golugwa, ambapo watu hao wametakiwa kujisalimisha katika vituo vya Polisi mara moja pindi waonapo taarifa hiyo popote pale walipo.



Prev Post Watu 172 Kortini Wakituhumiwa Kufanya Vurugu, Unyang’anyi Wa Kutumia Silaha Mwanza
Next Post Video: Msikilize Wakili Kibatala Akifanua Mashtaka yanayomkabili Niffer
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook