
 Wapiga kura visiwani Zanzibar leo, Jumanne Oktoba 28, 2025, wameanza zoezi la kupiga kura katika kile kinachofahamika kama kura ya mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika kesho, Oktoba 29, 2025, Tanzania Bara na Visiwani.
Wapiga kura visiwani Zanzibar leo, Jumanne Oktoba 28, 2025, wameanza zoezi la kupiga kura katika kile kinachofahamika kama kura ya mapema kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika kesho, Oktoba 29, 2025, Tanzania Bara na Visiwani.
Zoezi hilo linafanyika chini ya usimamizi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), ambapo vituo vya kupigia kura vimefunguliwa rasmi saa 1:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni, kwa saa za Afrika Mashariki.
Katika uchaguzi huo, Rais wa sasa wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anayetetea nafasi yake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), anakabiliana na Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, anayewakilisha Chama cha ACT Wazalendo.
Hata hivyo, chama cha ACT Wazalendo kimekuwa kikipinga uhalali wa kura ya mapema, kikieleza kuwa zoezi hilo linapaswa kufanyika kwa uwazi zaidi ili kulinda haki za wapiga kura wote.
Kwa mujibu wa taarifa za ZEC, matokeo ya urais wa Zanzibar yatatangazwa ndani ya saa 72 baada ya vituo kufungwa.
Kura ya mapema imekuwa ni utaratibu wa muda mrefu Zanzibar, ikilenga kutoa nafasi kwa vikundi maalumu kama askari wa usalama, maafisa wa uchaguzi na watumishi wa umma waliopangiwa majukumu maalumu siku ya uchaguzi mkuu.
 
  
 
 
   
             
             
	
                                             
                









 
                        
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!