Jumatano Oktoba 29, 2025, ni siku muhimu kwa Tanzania. Ni siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, tukio la kikatiba linalotazamwa kama kilele cha demokrasia ya taifa. Lakini mwaka huu, siku hiyo hiyo imechukua sura mbili. Wakati serikali na vyama vya siasa vinawahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura, makundi mengine yanayojitambulisha kama wanaharakati yanahamasisha maandamano, wakisema ni njia ya kupaza sauti zao dhidi ya kile wanachokiona kama kukwama kwa mageuzi ya kisiasa.
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw











Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!