Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

UJIO WA MERIDIANBET MBEZI WANUFAISHA WENGI….

  • 22
Scroll Down To Discover

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Meridianbet imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kurudisha kwa jamii kupitia kampeni zake za Uwajibikaji kwa Jamii. Katika kuunga mkono jitihada za kuhakikisha mazingira safi na salama, Meridianbet imekabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa wakazi wa Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na, mifagio, gloves, Reflectors, na vingine vingi ambapo hivi vyote vilipokelewa vizuri kabisa na Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Anna Lukindo mapema kabisa Jumamosi ya leo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwakilishi wa Meridianbet, ambaye pia ni Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo, Nancy Ingram baada ya kutoa vifaa hivyo aliweza kutoa neno akisema kuwa, “Meridianbet tunaamini kuwa usafi ni afya, na afya ni msingi wa maendeleo ya jamii. Kupitia zoezi hili, tunataka kutoa hamasa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira yao. Tunatambua jukumu letu kama sehemu ya jamii, na hii ni hatua mojawapo ya kuonesha kuwa tunajali,”

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbezi Juu ameishukuru Meridianbet kwa moyo wa kizalendo na ushirikiano wao katika kuunga mkono juhudi za serikali za mitaa katika kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama, safi, na yanayovutia.

Jumamosi ya leo chukua mzigo wako mapema ambapo mechi kibao zipo kwaajili yako siku ya leo. Suka jamvi lako la ushindi leo na ubashiri hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.

“Huu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kuhakikisha tunalinda afya na hadhi ya mazingira ya wananchi wetu. Tunatoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huu,” amesema Mh. Anna Lukindo.

Vifaa vilivyotolewa vitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mbezi Juu ili kusaidia ukusanyaji bora wa taka, kulinda usalama wa watoa huduma za usafi, na kuhimiza uwajibikaji wa pamoja katika kutunza mazingira.

Meridianbet inasisitiza kuwa itaendelea kurejesha kwenye jamii, kwani bila jamii wao si kitu, hivyo pia wanawasihi watu wengine na kampuni zingine kuiga mfano kutoka kwao kwani wenye uhitaji ni wengi sana.

 

The post UJIO WA MERIDIANBET MBEZI WANUFAISHA WENGI…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post UJIO WA MERIDIANBET MBEZI WANUFAISHA WENGI….
Next Post VODACOM YAZINDUA TWENDE BUTIAMA 2025 KWA LENGO LA KUBORESHA ELIMU, AFYA NA MAZINGIRA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook