MAGAZETI ya Leo Jumapili 20 April 2025
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, amezungumza kwa tahadhari kubwa kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, Aprili 20, 2025, akieleza kuwa wapinzani wao ni timu iliyo bora kiufundi, kimfumo na kiuchumi.
Davids amewasifu Stellenbosch kama klabu iliyopangika vizuri kuanzia juu hadi chini na inayojulikana kwa kuibua vipaji chipukizi licha ya kuuza wachezaji wao bora mara kwa mara.
“Ni klabu yenye nidhamu ya hali ya juu, wanauza wachezaji bora lakini bado wanaendelea kusajili vipaji vijana. Ni timu hatari ambayo hatuwezi kuichukulia poa hata kidogo,” amesema Fadlu.
Kocha huyo amesema kila timu iliyofika hatua ya nusu fainali inastahili kuheshimiwa, na hivyo Simba inajiandaa kwa umakini mkubwa kuhakikisha wanafuzu kwenda fainali.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!